Featured

TATIZO LA MINYOO KWA MBUZI/KONDOO NA NAMNA YA KUTIBU

Utangulizi

Minyoo huishi tumboni katika kondoo na mbuzi. Minyoo hii hutaga mayai ambayo hutolewa kupitia kinyezi chao kisha hukua hadi kiwango cha larvae kwenye mifugo.

 


Jinsi ya kutambua mifugo wenye minyoo

 • Uchovu na kukosa hamu ya kula.
 • Ngozi zenye nywele zilizojikita.
 • Macho kukosa rangi ya kawaida.
 • Uvimbe unaoning’inia chini bottele jaw.’
 • Hali dhaifu ya mwili.
 • Kuhara kutegemea mdudu anayeathiri
 • Vifo hutokea kwenye hali mbaya.

 


Umuhimu wa tiba mwafaka

 • Tiba mwafaka itachangia:
 • Afya nzuri ya mifugo.
 • Uambukizi haba malishoni.
 • Kutozoeana na dawa mwilini hadi zikose kufanya kazi.

Jinsi ya kuhakikisha tiba mwafaka

 • Tibu mifugo wote wakati nyasi imebadilika rangi ya hudhurungi wakati wa kiangazi ili kuzuia maradhi sugu.
 • Tumia dawa ambayo itaua minyoo iliyokaa kitako na urudie tiba baada ya wiki mvua inyeshapo.
 • Kuwapa mifugo mawe ya molasses yenye mbolea ya urea ambayo ina dawa inasaidia kuimarisha hali ya afya mbali na kusaidia katika kutibu.
 • Tibu ili kukatisha maisha kamili ya wadudu.
 • Tumia kiwango cha dawa kifaacho,   ukilinganisha na uzito wa kila mfugo au uzito wa mfugo aliye mzito Zaidi katika kundi.        
 • Tia dawa juu ya ulimi kuhakikisha dawa imepenya ipasavyo hasa asubuhi kabla ya mifugo kuamsha kinywa
 • Kama mfugo amezoea dawa, mpe viwango viwili vya dawa zikifuatana kwa masaa kumi na mawili.
 • Wape mbuzi dawa mara  moja  na nusu Zaidi ya kiasi   kinachopewa kondoo.

 


Ni changamoto gani hutokea hata baada ya tiba mwafaka?

Kiasi cha mifugo

Kufuga Zaidi ya mifugo watano kwenye eka moja ya malisho kunachangia kuambukizana na hivyo kunaleta kujirudia kwa maradhi.

 

Kutobadilisha sehemu za malisho

Kubadilisha malisho hupunguza kujirudia kwa maambukizi ya minyoo.

 

Mahali pa jamii pa kunywesha mifugo na malisho ya barabarani

Hizi ni sehemu ambapo mifugo huokota minyoo.

 

Ni mbinu gani zingine za kupunguza uambukiza wa minyoo?

 • Kama mifugo wanalishwa ndani ya hori, sakafu iwe imeinuliwa.
 • Vyombo vya lishe na maji vijengwe kwenye kuta kuzuia kinyezi kuanguka ndani.      
 • Mifugo wapewe chakula cha kiasi na hali bora inayofaa.
 • Wape dawa za minyoo mifugo wanaonunuliwa masaa arobaini na nane kabla ya kuwaleta shambani kwako.
 • Fuga mifugo wanaojulikana kustahimili minyoo.

 

Mifugo wanahitaji tiba mara ngapi?

 • Hii itategemea hali ya anga na mazingira yako.  

 

Sehemu za Pwani na ziwa la Victoria 

 • Mayai huanguliwa haraka lakini hufa ajili ya joto jingi.
 • Tibu wanyama wote kabla ya msimu wa mvua.  
 • Kuhamisha pahali pa kufunga baada ya siku tatu kunasaidia

 

Sehemu kame na zile kame kiasi

 • Minyoo michanga inayomezwa wakati wa kiangazi inaweza kukaa kitako na kukua mvua inyeshapo. 
 • Nyakati zingine za mwaka ni kavu sana kiasi cha minyoo kutostahimili lakini maambukizi yanaendelea kwa vinywesho za maji na bomani.

 


Subscribe to this Blog via Email :