Featured

FAIDA NA UMUHIMU WA VITAMIN KWA KUKU🐓

UKOSEFU  wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin.

📌 UMUHIMU WA VITAMINI.
– Husaidia katika ukuaji wa kuku.
– Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka.
– Husaidia kuku kuwa mwenye afya.
– Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri.
 
📌 UKOSEFU WA VITAMIN ‘A’ KWA KUKU
Ukosefu wa vtamin ‘A’ hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin ‘A’ kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa kwa ukosefu wa vitamun ‘A’ pia hata kuku wakubwa.
 
📌 DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN ‘A’ KWA KUKU
-Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji
-Hudhoofika na hatimaye kufa

📌 TIBA NA KINGA
-Kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani
-Wape kuku vitamini za kuku za dukani wakati majani hayapatikani
-Kwa kuku alie athirika na ugonjwa huu msafishe na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi hakikisha uchafu wote unatoka kisha mpe vitamin ya dukani… Fanya zoezi hilo kwa siku 5.

 
📌 VITAMINI B
Manyoya huonekana kusambaratika, panga za kuku kuonekana zikiwa zimepauka, na kwa kuku watagaji hupunguza uwezo wao wa kutotoa mayai.
 
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Wapatie kuku wako Dawa za multivitamin.
 
📌 VITAMIN E
Hizi ni dalili za ukosefu wa vitamin E kwa kuku,
– shingo huanguka chini na kupinda.
– Vifaranga huanguka kifudi fudi.
– Utagaji wa kuku hushuka kwa kiasi kikubwa.
 
📌 VITAMIN D
Ukosefu wa vitamin D hupelekea tatizo la mifupa kuwa laini, na hali hii hupelekea mifupa kupinda pia magoti huvimba na hata midomo kuwa laini. Na hata ukuaji wa kuku huwa wa hafifu. Hii hutokana madini aina ya madini ya calcium na fosifolusi kutojengeka kwenye mifupa.
Kwa kuku watagaji hali hii hupeleka kwa kuku watagaji kutaga mayai yenye ganda laini.
 
📌JINSI YA KUKABILIANA.
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mimea, mfano majani ya lusina, mpapai, mchicha na mikunde
Kazi ya vitamini ni kulinda mwili dhidi ya magonjwa, watu wengi hupenda kutumia vitamini mbadala za viwandani kuliko zile vitamini halisia ambayo imetokana na nguvu za jua na madini toka kwenye udongo ambayo hupatikana kwenye majani, ni vyema ukaangalia vitu vinavyopatikana katika eneo lako ili kutengeneza chakula cha mifugo yako

Subscribe to this Blog via Email :