Featured

JINSI YA KUKAGUA UBORA WA KIFARANGA

1. Uchangamfu
mgeuze kifaranga alalie mgongo wake na kupima ni jinsi gani na kwa haraka ataweza kugeuka na kusimama na miguu yake.

2. Kitovu 
kitovu cheusi, uwazi wa kitovu, kitovu kamba, kitovu kichafu na ngiri. Kitovu cha kifaranga bora lazima kiwe kimeshapona.

3. Miguu 
kusiwepo uvimbe kwenye miguu ya kifaranga

4. Mdomo
usiwe na majimaji au unyevunyevu. Pia kagua pua kama ni safi.

5. Tumbo 
liwe laini kwa kugusa na lisiwe na uvimbe au ugumu.
Katika zoezi zima la ukaguzi hakikisha kuwa vifaranga wanashikwa kwa uangalifu mkubwa sana. Ni rahisi kumuumiza kifaranga akiwa mdogo.

Imeandaliwa na mtaalamu wa UFUGAJIMAKINI

Subscribe to this Blog via Email :